
KINACHOONEKANA
kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya
maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa kubadilika na
kuona ugonjwa huo ni wa kawaida kama ilivyo kukohoa au kichwa kugonga.
Hilo limedhihirika baada ya juzi chanzo chetu cha habari kupasha
kwamba, baadhi ya wafanyabiashara na wabunge wameingia ‘kazi’ ya
kuwanasa mastaa wa kike Bongo, hasa waigizaji wa filamu.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wafanyabiashara maarufu wa jijini Dar...